Wanajeshi 25 wahukumiwa kifo Kongo
4 Julai 2024Matangazo
Kwa mujibu wa mawakili wao, kesi hiyo iliwajumuisha watuhumiwa 31, wakiwemo wanajeshi 27 na wanne kati ya wake zao.
Kesi hiyo iliendeshwa kwenye mahakama ya kijeshi ya Butembo, karibu na mstari wa mbele wa mapambano.
Soma zaidi: Wanne wauawa, 25 wajeruhiwa kwa mabomu ya M23
Miongoni mwa mashitaka waliyoshitakiwa nayo yalikuwa ni kuharibu silaha za kivita, kukaidi amri halali na wizi, ambapo wanajeshi 25, wakiwemo makapteni wawili, walihukumiwa kifo.
Waliosalia, wakiwemo wake zao, waliachiwa huru kwa kukosekana ushahidi. Kundi la M23 limetwaa udhibiti wa miji kadhaa muhimu , ukiwemo mji wa kimkakati wa Kanyabayonga, unaounganisha miji miwili ya kibiashara ya Butembo na Beni.