Kama ilivyo kwa nchi nyingi za kiafrika, uchafuzi wa mazingira ni tatizo sugu kwa Msumbiji. Athari za kukosekana mfumo mzuri wa ukusanyaji taka zinadhihirika kwenye pwani ya Mashariki ambako kuna mlundikano wa taka, nyingi zikiwa zile zilizotupwa na waliokuja kutembea. Mtaalamu wa sheria na mazingira Carlos Serra Junior ameamua kuchukua hatua.