1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanafunzi wataka vyuo vikuu vifungwe

Sylvia Mwehozi
7 Oktoba 2016

Wanafunzi wanaopinga ongezeko la gharama za ada nchini Afrika Kusini wametaka vyuo vikuu vyote vifungwe hadi pale serikali itakaporuhusu elimu bure kwa kila mwanafunzi katika taifa hilo kubwa la kusini.

https://p.dw.com/p/2R0Rp
Südafrika Proteste Studenten Universität
Picha: picture-alliance/dpa/AP/T. Hatebe

Maandamano ya wanafunzi wanaopigania usawa kwenye fursa ya kupata elimu yamevilazimisha baadhi ya vyuo vikuu, vikiwemo Witswatersrand na Cape Town, kuahirisha masomo mara mbili katika kipindi cha mwezi mmoja.

Chuo Kikuu cha Wits kilitarajiwa kuanza tena masomo hapo Jumatatu (3 Oktoba), lakini kukatokea mapambano kati ya wanafunzi na polisi katika kampasi ya chuo hicho.

Katika taarifa yake, chuo hicho kilisema kwamba hakikufikia makubaliano na wanafunzi waliokuwa wakiandamana juu ya kuanza tena kwa masomo siku ya Jumatatu inayofuata (Oktoba 10).

Gharama za elimu ya juu inayopingwa na wanafunzi wengi weusi imekuwa kiashiria cha kutokuwepo kwa usawa unaoendelea kuikumba Afrika Kusini kwa zaidi ya miongo miwili baada ya kumalizika kwa mfumo wa ubaguzi wa rangi nchini humo.