DW imezungumza na mwanafunzi aliyekuwa akichukua kozi ya udaktari mjini Kyiv Aiman Hassan Vuwai ambaye amewasili mjini Budapest, anaelezea hisia zake aliposikia serikali yake ipo kwenye utaratibu wa kuwatoa katikati ya mapambano ya wanajeshi wa Urusi na Ukraine.