1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wamahiaji 500 waokolewa karibu na Canary

20 Septemba 2024

Mamlaka nchini Uhispania zimesema meli za uokoaji zimewaokoa usiku wa kuamkia leo karibu na visiwa vya Canary, wahamiaji takriban 500 waliokuwa wakitokea barani Afrika.

https://p.dw.com/p/4kuYL
Mashua ikiwa na wahamiaji karibu na visiwa vya Canary.
Mashua ikiwa na wahamiaji karibu na visiwa vya Canary.Picha: Europa Press/AP Photo/picture alliance

Zaidi ya watu 300 waliokolewa na meli ya uokoaji ya Guardamar Calliope na kupelekwa kwenye mji wa bandari wa La Restinga kusini mwa kisiwa cha El Hierro, huku wahamiaji wengine wakipelekwa katika Visiwa vya Canary vya La Gomera na Lanzarote.

Soma zaidi: Uholanzi inataka kujiondoa katika kanuni za uhamiaji za Ulaya

Maelfu ya wahamiaji hasa kutoka pwani ya nchi za Afrika Kaskazini na Magharibi wamekuwa wakiwasili katika visiwa hivyo vya Uhispania huku mamia ya wengine wakifa maji wakati wakijaribu kuingia Ulaya.