1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Waliofariki tetemeko la ardhi nchini Morocco yafika 2,901

12 Septemba 2023

Mamlaka nchini Morocco imesema leo kuwa watu 2,901 wamepoteza maisha katika tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika huku matumaini ya kupata manusura zaidi yakipungua.

https://p.dw.com/p/4WFyk
Timu ya waokoaji ikishusha masanduku ya mahitaji ya muhimu
Timu ya waokoaji ikishusha masanduku ya mahitaji ya muhimuPicha: AFP/Getty Images

Takriban watu 5,530 wamejeruhiwa katika tetemeko hilo la ardhi la 6.8 kwenye kipimo cha Ritcha lililoipiga Morocco siku ya Ijumaa. 

Wizara ya mambo ya ndani imeongeza kuwa, shughuli za uokoaji bado zinaendelea japo kwa kasi ndogo huku mamlaka ikifanya juhudi za kufungua barabara zilizoharibika au kufungwa.

Soma pia:Msalaba Mwekundu waitisha misaada zaidi Morocco

Morocco imekubali misaada kutoka kwa Uhispania, Qatar, Uingereza na Umoja wa Falme za Kiarabu UAE.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto la UNICEF limesema ripoti za awali zinaonyesha kuwa, takriban watoto 100,000 wameathirika na tetemeko hilo la ardhi.