1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa watangaza kuondoka Mali

14 Agosti 2023

Ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali umetangaza kuondoka mapema kutoka kwenye kambi yake iliyoko kaskazini mwa nchi hiyo

https://p.dw.com/p/4V7q8
Mali | MINUSMA Mission der Vereinten Nationen
Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Hatua hiyo inatokana na kuzorota kwa usalama.Ujumbe huo wa MINUSMA umesema kwenye taarifa yake kwamba pamoja na mazingira tete ya usalama, lakini pia kikosi chake kinakabiliwa na kitisho kikubwa.Kwa siku chacvhe zilizopita muungano wa waasi unaoongozwa na kabila ya Tuareg umevituhumu vikosi vya Mali na wapiganaji wa kundi binafsi la Wagner la nchini Urusi kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano kwa kuvishambulia vikosi vyake vilivokuwepo karibu na Ber.Jeshi la Mali halijasema chochote juu ya tuhuma hizo.