1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliberia kushiriki kura ya maoni kupunguza mihula ya urais

8 Desemba 2020

Waliberia wanashiriki leo katika zoezi la kura ya maoni kuhusu mpango wa Rais George Weah wa kupunguza mihula ya urais, huku wakosoaji wakihofia kuwa anaweza akayatumia mabadiliko hayo kubakia madarakani.

https://p.dw.com/p/3mOmU
Äthiopien Addis Abeba Afrikanische Union Gipfel Guterres George Weah
Picha: Reuters/T. Negeri

Nguli huyo wa zamani wa kandanda Weah amewaambia wafuasi wake kwamba kubaki na kiongozi mmoja madarakani kwa miaka mingi sio kitu kizuri na anataka marais na wabunge kuhudumu kwa miaka mitano badala ya sita, na maseneta kuhudumu kwa miaka saba badala ya nane. Wanasiasa wa upinzani Liberia wanahofia kuwa Weah, mwenye umri wa miaka 54, huenda akajaribu kubakia madarakani isipokuwa ofisi yake inakanusha madai hayo. Kando na kura ya maoni ya kupunguza mihula ya marais na wabunge, Waliberia pia wanaamua kama waondoe marufuku iliyowekwa mwaka wa 1973 kuhusu uraia wa nchi mbili, hatua ambayo baadhi ya watu wanatumai huenda ikawa neema ya kiuchumi katika taifa hilo maskini lenye idadi ya watu milioni 4.8