1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakuu wa SADC kukutana Namibia kujadili usalama wa DRC

8 Mei 2023

Maazimio kutoka mkutano huo yanatarajiwa kutoa mchango katika juhudi za bara la Afrika kutafuta suluhisho la kudumu kwa tatizo sugu la ukosefu wa usalama mashariki mwa Kongo.

https://p.dw.com/p/4R2LI

Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Ukanda wa Kusini mwa Afrika, SADC wanakutana leo Jumatatu katika mji mkuu wa Namibia, katika mkutano maalumu wa kilele kujadili hali ya usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Maazimio kutoka mkutano huo yanatarajiwa kutoa mchango katika juhudi za bara la Afrika kutafuta suluhisho la kudumu kwa tatizo sugu la ukosefu wa usalama mashariki mwa Kongo.

Shirika la utangazaji la Afrika Kusini, SABC limeripoti kuwa rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa, ni miongoni mwa marais watakaoshiriki katika mkutano huo.

Ramaphosa ambaye anamaliza muda wake kama mwenyekiti wa kitengo cha siasa, ulinzi na ushirikiano wa kiusalama katika jumuiya ya SADC, anaambatana na waziri wake wa mambo ya nje na waziri wa ulinzi.