1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiVatican

Wakristo washerehekea Krismasi ulimwenguni kote

25 Desemba 2023

Waumini wengi wa Kikristo ulimwenguni kote wanasherehekea Sikukuu ya Krismasi Jumatatu, huku kiongozi wa Kanisa Katoliki akihimiza amani na huruma.

https://p.dw.com/p/4aYpl
Vatikan Petersdom 2023 | Papa Francis
Papa Francis akiwasilia kwa ajili ya Misa ya Krismas katika uwanja wa Mt. Peter mjini Vatikan, Desemba 25, 2023.Picha: Tiziana Fabi/AFP/Getty Images

Kiongozi wa kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis anatarajiwa kuwasilisha ujumbe wake wa kitamaduni wa Krismasi katika kanisa mkuu wa Mtakatifu Petero huko Vatican.

Kwenye ujumbe wake, Papa Francisanatarajiwa kukemea vita na ghasia, hasa ikizingatiwa sherehe za mwaka huu zinafanyika wakati kuna umwagaji damu kutokana na vita kama vya Gaza na Ukraine.

Soma pia: Steinmeier: Sote tunamani ulimwengu wa amani zaidi

Lakini mjini Bethlehemu, alikozaliwa Yesu Kristo, hali ni tofauti. Ulinzi mkali umewekwa na majeshi ya Israeli.

Viongozi wa Kikristo pia wameamua kuachana na mapambo ya Krismasi katika eneo hilo takatifu kwa sababu ya vita.