Wakimbizi wa Rohingya waandamana kupinga hali duni ya maisha
31 Mei 2021Matangazo
Kulingana na polisi karibu watu 4000 wameshiriki maandamano hayo na yamefanyika wakati ambapo kulikuwa na ziara ya maafisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR.
Mtu mmoja wa kabila la Rohingya ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa waandamanaji wamerusha mawe na polisi waliwazuia kuingia katika jengo ambamo maafisa wa UNHCR walikuwemo.
soma zaidi: Kundi la kwanza la wakimbizi wa Rohingya lawasili kisiwa cha Bangladesh
Tangu Desemba, Bangladesh imewahamisha wakimbizi 18,000 na kuwapeleka katika kisiwa hicho cha Bhashan Char kilicho katika eneo la chini ambapo idadi jumla ya watu 850,000 wanaishi katika hali duni.
Bangladesh inapania kuwahamisha wakimbizi laki moja na kuwapeleka katika kisiwa hicho.