Wakimbizi wa DRC wakimbilia Rwanda
25 Oktoba 2022Katika tangazo lake mbele ya vyombo vya habari mjini Goma,msemji wa jeshi jenerali sylvain Ekengeameeleza kua bado mapigano makali yanaendelea katika baadhi ya vijiji wilayani Rutshuru ikiwemo Ntamugenga ambamo alilituhumu kundi la M23 kuwauwa raia zaidi ya watatu na kuwajeruhi wengine kadhaa kwa risasi.
Wakati huo huo, hali ilikuwa ya wasiwasi jana (Jumatatu) kutwa katika mji mdogo wa Rubare kwenye barabara inayo elekea Goma ambamo wananchi walilazimika kuanza kufunga maduka na wengine kukimbia baada yakuanguka kwa bomu ndani ya bwawa la kufugia samaki nje kidogo na mji huo. katika mahojiano maalumu na idhaa hii , meja Willy Ngoma msemaji wa kundi la waasi wa M23 ambaye amekiri pia ongezeko la vifo vya raia tangu kuzuka kwa mapigano hayo amekuwa na haya yakujulisha.
Kwa sasa karibu eneo lote linalo dhibitiwa na waasi ikiwemo Ntamugenga limebaki bila wakaazi ambao baadhi wamekimbilia katika maeneo yanayo dhaniwa kuwa tulivu.
Soma zaidi:Tshisekedi aiandama Rwanda Umoja wa Mataifa
Hata hivyo, kulingana na ripoti ya ofisi ya umoja wa mataifa yakuratibu masuala ya kibinadamu, OCHA, wakimbizi zaidi ya elfu 20 wamelikimbia wimbi hili jipya la mapigano katika wilaya ya Rutshuru huku zaidi ya wengine 2500 wakiuvuka mpaka kuelekea katika nchi jirani ya Uganda tangu kuzuka kwa mapigano hayo.
DW: DRC