1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi 200,000 nchini Tanzania kupunguziwa chakula

31 Mei 2023

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP limesema kuwa zaidi ya wakimbizi 200,000 nchini Tanzania watapokea nusu tu ya mgao wa chakula kuanzia mwezi ujao kwa sababu ya ukosefu wa pesa za wafadhili.

https://p.dw.com/p/4S0MT
Picha hii ya Aprili 25, 2021 inaonyesha wakimbizi wa Burundi waliokimbilia nchini Tanzania
Picha hii ya Aprili 25, 2021 inaonyesha wakimbizi wa Burundi waliokimbilia nchini TanzaniaPicha: Yakub Talib/DW

Taarifa iliyotolewa jana na WFP imeeleza kuwa mgao wa chakula kwa wakimbizi Tanzania, ambao asilimia 70 ni kutoka Burundi na waliobakia wanatoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, umepunguzwa kwa kasi tangu mwaka 2020. Kwa mujibu wa WFP, mwezi Juni, mgao utapungua kwa asilimia 50, hali inayoweza kuwaacha maelfu ya wakimbizi wakihangaika kukidhi mahitaji yao ya lishe. Shirika hilo limebainisha kuwa dola milioni 21 zinahitajika haraka ili kuepuka kupunguza zaidi mgao wa chakula. Mkurugenzi wa WFP nchini Tanzania, Sarah Gordon-Gibson amesema shirika hilo lina wasiwasi mkubwa kwamba upunguzaji huo utawalazimisha wakimbizi kuingia katika mazingira magumu zaidi.