Wajumbe wa Kipalestina wakataa kwenda Geneva:
30 Novemba 2003Matangazo
RAMALLAH: Siku moja kabla ya kusainiwa aina ya Mpango wa Amani wa Mashariki ya Kati, wajumbe wawili muhimu wa Kipalestina wamesema hawatohudhuria sherehe hiyo mjini Geneva. Sababu za uamuzi huo wa Mawaziri wa Kipalestina Kadura Fares na Muhammed Horani ni kwamba hayo yaitwayo MAPATANO YA GENEVA yanapingwa vikali na chama cha FATAH, ilisema taarifa ya Kipalestina. Mapatano hayo yaliyokuwa yasainiwe mjini Geneva Jumatatu ya kesho, yalifikiwa kati ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Habari wa Kipalestina, Yassir Abeid Rabbo na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Sheria wa Israel, Yossi Beilin. Mapatano hayo yalisisitiza pia kuundwa kwa taifa ya Kipalestina. Upande wa pili, mapatano hayo yanashikilia kuwa familia za Wapalestina waliofukuzwa kwao, wasamehe haki ya kurudi kwao.