1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajerumani walio nje wamehimizwa kupiga kura Februari 23

28 Desemba 2024

Ujerumani inawataka raia wanaoishi nje ya nchi mara moja kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ikiwa wanataka kushiriki katika uchaguzi ujao utakaofanyika Februari 23.

https://p.dw.com/p/4odsV
Entscheidung zur Auflösung des Deutschen Bundestages
Rais wa Shirikisho Frank-Walter Steinmeier akitangaza uamuzi wa kulivunja Bunge la Ujerumani.Februari 23 mwaka ujao.Picha: Soeren Stache/dpa/picture alliance

Duru zinaeleza maombi ya usajili tayari yanaweza kuwasilishwa kwa mamlaka za ndani. Wajerumani wanaoishi nje ya nchi wamewekwa katika kundi la raia ambao hawajasajiliwa nchini Ujerumani. Jana Ijumaa, Rais wa UjerumaniFrank-Walter Steinmeier alivunja bunge na kuitisha uchaguzi wa mapema Februari 23, ikiwa ni miezi saba kabla ya tarehe iliyopangwa awali. Uamuzi huo unatokana na kuporomoka kwa muungano wa vyama vitatu uliyokuwa inaongozwa na Kansela Olaf Scholz mwezi Novemba na  kufuatiwa na kura ya imani Desemba 16.