Wajasirimali wa kiafrika – Wenye mafanikio na wenye kuwajibika
10 Mei 2012Katika mfululizo huu tunawatambulisha wajasiriamali kutoka Afrika waliobobea katika kazi yao na ambao baada ya safari ndefu hatimaye wamekuwa wafanyabiashara wenye mafanikio. Tutamtembelea mtengenezaji wa michezo ya watoto kutoka Afrika Kusini, mtu aliyeleta mageuzi ya vyoo nchini Kenya, mfanyabiashara mkubwa katika sekta ya mawasiliano kutoka Sudan anayeishi London, Uingereza na wengine wengi. Hawajafanikiwa katika kazi zao tu bali pia wanarudisha sehemu ya mafanikio yao katika jamii kwa namna moja au nyingine.
Wajasiriamali wetu wanazungumza wazi juu ya changamoto walizokumbana nazo katika kuelekea kwenye tabaka la juu la jamii, vikwazo vilivyowakumba na kile kilichowapa moyo. Kupitia simulizi zao pamoja na uzoefu wao, wasikilizaji watafahamu jinsi ya kujiajiri wenyewe pamoja na nafasi abazo ajira hiyo inaleta kwa mtu binafsi na hata kwa ukuaji wa uchumi wa taifa.
Vipindi vya Deutsche Welle “Learning by Ear – Noa Bongo! Jenga Maisha Yako” vinapatikana katika lugha sita: Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamharic.