Wairan waelekea vituoni kumchagua rais mpya kumrithi Raisi
28 Juni 2024Licha ya cheo cha rais, Raisi alikuwa nambari mbili katika muundo wa mamlaka ya Iran kwa kuwa Kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khameneianahudumu kama mkuu wa nchi na ndiye mwenye uamuzi wa mwisho katika masuala yote ya kimkakati. Pia ni kamanda mkuu wa majeshi ya Iran. Baraza la Ulinzi, ambalo ni chombo cha usimamizi cha kihafidhina, kiliwaidhinisha wagombea sita pekee kwa uchaguzi huo.
Soma pia: Iran kupiga kura ya urais siku ya Ijumaa
Mapema wiki hii, wagombea wawili wa kihafidhina wenye msimamo mkali walijiondoa kinyang'anyironi katika juhudi za kuunganisha uungwaji mkono miongoni mwa wapiga kura wenye misimamo mikali. Hii ina maana ni wagombea wanne waliobaki katika uchaguzi wa kumrithi Raisi.
Wagombea wanaoonekana kuwa na nafasi nzuri zaidi za kushinda ni Saeed Jalili, mwenye msimamo mkali, mpatanishi wa zamani katika mazungumzo ya kimataifa ya nyuklia, na spika wa bunge Mohammad Bagher Ghalibaf, pamoja na waziri wa zamani wa afya na mwanamageuzi Masoud Pezeshkian. Iwapo hakuna mgombea atakayepata wingi mkubwa wa kura, duru ya pili ya uchaguzi utafanyika Julai 5.