Wahouthi washambulia meli nje ya pwani ya Kusini mwa Yemen
12 Februari 2024Shirika la shughuli za usafiri wa majini la Uingereza UKMTO limesema tukio hilo limetokea alfajiri na wafanyakazi wa meli hiyo wameripotiwa kuwa salama wakati meli hiyo ikiendelea na safari yake kuelekea kwenye bandari nyingine.
Shirika jingine la masuala ya usalama la Ambrey limesema meli hiyo iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Jamhuri ya visiwa vya Marshall na inayomilikiwa na kampuni moja ya Ugiriki ililengwa kwa makombora katika matukio mawili tofauti ndani ya kipindi cha dakika 20.
Soma pia: Waasi wa Houthi wa nchini Yemen wazidisha mashambulizi katika Bahari ya Shamu
Mmiliki wa meli hiyo ni miongoni mwa walioko kwenye soko la hisa la Marekani NASDAQ. Waasi wa Kihouthi wamekuwa wakizilenga meli zinazipita katika bahari ya Sham tangu mwezi Novemba na kusababisha mashambulizi ya kupiza kisasi ya Uingereza na Marekani.