1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahouthi waripoti kifo cha kwanza cha raia

26 Februari 2024

Wapiganaji wa Kihouthi nchini Yemen wanaoungwa mkono na Iran wameripoti kifo cha kwanza cha raia katika mashambulizi ya anga ya hivi karibini yaliyofanywa Marekani na Uingereza mwishoni mwa wiki.

https://p.dw.com/p/4csoU
Msemaji wa kijeshi wa kundi la Wahouthi, Yahya Saree.
Msemaji wa kijeshi wa kundi la Wahouthi, Yahya Saree.Picha: XinHua /dpa/picture alliance

Shirika rasmi la habari la Yemen (SABA) limenukuu taarifa ya wizara ya afya iliyoripoti kuhusu kifo hicho jioni ya Jumapili (Februari 25) kilichotokea katika wilaya ya Maqbana jimboni Taiz, siku moja baada ya vikosi vya Marekani na Uingereza kusema vimeshambulia maeneo 18 kote nchini humo.

Mashambulizi hayo ya Marekani na Uingereza yanajibu mashambulizi ya droni na makombora ya waasi hao wa Kihouthi dhidi ya meli zinazopitia Bahari ya Shamu tangu mwezi Novemba.

Wapigaaji wa Kihouthi wanadai wanafanya mashambuizi dhidi ya meli hizo kuonesha mshikamano wao na Wapalestina katika vita vya Gaza.