Wahouthi waizamisha meli ya mizigo Bahari ya Shamu
19 Juni 2024Matangazo
Kulingana na Shirika la Operesheni za Baharini la Uingereza (UKMTO), meli hiyo ya MV Tutor iliyokuwa na bendera ya Liberia na inayomilikiwa Ugiriki, ililengwa na droni kutoka baharini katika eneo la Hodeida mnamo Juni 12.
Meli hiyo ni ya pili kuzamishwa na Wahouthi katika miezi ya hivi karibuni baada ya meli ya Rubymar, ambayo ilikuwa imebeba maelfu ya tani ya mbolea.
Soma zaidi: Wafanyakazi tisa wa UN washikiliwa na Waasi wakihouthi Yemen
Meli hiyo ilizama katika Bahari ya Shamu mnamo mwezi Machi baada ya shambulizi la kombora.
Waasi wa Kihouthi wamekuwa wakifanya mashambulizi ya droni na makombora katika njia muhimu ya Bahari ya Shamu tangu mwezi Novemba, wakisema wanalipiza kisasi kwa vita vya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza.