1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahanga wa operesheni ya kijeshi ya Israel Jenin wafikia 10

4 Julai 2023

Idadi ya waliouwawa tangu jeshi la Israel lilipoanzisha operesheni kubwa ya kuwasaka wanamgambo wakipalestina,katika eneo la Ukingo wa Magharibi,imefikia watu 10.

https://p.dw.com/p/4TO0A
Westjordanland Region Dschenin | Israelische Militäroperation | Palästinensische Jugendliche
Picha: Jaafar Ashtiyeh/AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa wizara ya afya mjini Ramallah, mwili wa Mpalestina mmoja ukiwa na majeraha ya risasi ulipatikana usiku wa kuakia leo, huku watu 100 wakiwa wamjeruhiwa, 20 wakiwa katika hali mahututi.

Israel ilianzisha operesheni kubwa ya kijeshji ambayo haijawahi kuonekana katika kipindi cha muongo mmoja katika Ukingo wa Magharibi jana Jumatatu.

Wanajeshi 1,000 waliingia kwenye mji wa Jenin na kukabiliana kwa masaa chungunzima na wapalestina waliojihami.

Kwa mujibu wa jeshi la Israel, operesheni yao inayoendelea, inalenga miundo mbinu ya wanamgambo wakipalestina.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW