Wahanga wa Ongwen kulipwa yuro milioni 52
29 Februari 2024Matangazo
Majaji wanesema Ongwen ambaye alikuwa mmoja wa makamanda wakuu wa waasi wa Lords Resistance Army, LRA, hana raslimali za kulipa fidia hiyo mwenyewe.
Badala yake wametaka fedha hizo zitolewe kutoka kwenye Mfuko wa Wahanga wa mahakama hiyo ambapo kila mhanga atapokea malipo ya yuro 750.
Ongwen alifunguliwa mashtaka na kuhukumiwa kifungo cha miaka 25 jela mwaka 2021 baada ya kupatikana na hatia katika visa 60 vya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwemo ubakaji, mauaji na utekaji nyara watoto. Kwa sasa anahudumia kifungo chake nchini Norway.