1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji zaidi waingia UK kwa boti

22 Agosti 2024

Wahamiaji 13,489 waliingia Uingereza kwa boti katika nusu ya kwanza ya mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4jnh7
Wahamiaji wakivuka ujia wa bahari wa English Channel.
Idadi ya wahamiaji wanaoingia Uingereza kupitia njia ya bahari kati ya nchi hiyo na Ufaransa imengezeka pakubwa katika nusu ya kwanza ya 2024.Picha: Dan Kitwood/Getty Images

Idadi ya wahamiaji waliowasili Uingereza kwa boti kupitia ujia wa bahari unaofahamika kama English Channel imefikia watu 13,489 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu 2024.

Idadi hiyo inatajwa kuwa kubwa zaidi katika muda wa miezi sita ya kwanza mwaka huu.

Takwimu za wizara ya mambo ya ndani zilizotolewa leo zimeonyesha ongezeko la asilimia 18 tofauti na mwaka uliopita ambapo wahamiaji 11,433 walifanya safari hiyo hatari kati ya mwezi Januari hadi Juni mwaka 2023.

Papo kwa Papo 27.06.2016

Soma pia: Uingereza yathibitisha kuwazuia wahamiaji

Raia wa Afghanistan wanajumuisha asilimia 18 ya wahamiaji waliowasili nchini humo katika kipindi hicho cha miezi sita, wakifuatiwa na Wairan kwa asilimia 13, Vietnam asilimia 10, Waturuki asilimia 10 na Wasyria kwa asilimia tisa.

Takwimu hizo zinaonyesha ni kwa namna gani serikali mpya ya Leba nchini Uingereza inavyokabiliwa na changamoto ya uhamiaji hasa wakati huu ambapo inajaribu kukabiliana na wimbi la wahamiaji lililosababisha hasira ya umma.