1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UtamaduniTanzania

Wahadzabe: Tunapenda na kulinda utamaduni wetu wa jadi

Veronica Natalis
9 Agosti 2023

Jamii ya Wahadzabe ni moja kati ya makabila yaliyobaki duniani yanayoendeleza utamaduni wa kale, ikiwa pamoja na shughuli za uwindaji,kula matunda, mizizi na aina mbalimbali za wanyama kwa miaka zaidi ya elfu elfu 40.

https://p.dw.com/p/4UwkH
Brasilien Pororoca-Surf-Festival
Picha: Eraldo Perez/AP Photo/picture alliance

Ni miongoni mwa jamii chache duniani ambazo zinalinda utamaduni wale, lakini mabadiliko ya hali ya hewa ni tatizo, kwa tamaduni hiyo kuendelea kuhifadhi mwenendo wake wa maisha.

Wanaume hasa kazi yao kubwa ni uwindaji wa Wanyama, kuchimba mizizi na kutafuta matunda na asali kwa ajili ya chakula.

Nashuhudia wanawake wakijishughulisha na shughuliza mikono kama vile kutengeneza shanga na uchongaji wa vinyago na mapambo ya aina mbali mbali.

Soma pia:Serikali ya Kenya yaanza mchakato wa kuifidia jamii asilia na ya wachache ya Ogiek

Wanaishi kwenye nyumba za nyasi na maisha yao ni tofauti kabisa na Maisha ya jamii za watu wengine nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Jamii hiyo kadhalika ambayo kwa kiwango kikubwa imekuwa ikitegemea mazao ya misitu kuendesha masiha, wanasema mabadiliko ya Tabia nchi zinatishia usalama wao.

"Hatupati Wanyamapori wa kutosha kutokana na ukame wa muda mrefu,"

Alisema huku akionesha namna ambavyo jamii za wafugaji zinavyoingiza mifugo katika maeneo ya pori tengefu ambayo jamii hiyo ni sehemu yake.

 "Shughuli za kibinadamu nazo zimechangia kwa kiasi kikubwa,"

Alisema hatiua hiyo imesababisha wanyama kuhama na kwenda mbali zaidi hatua inayosababisha upatikanaji wake kuwa mgumu.

Vijana wanajivunia jamii yao

Kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 17 kutoka jamii hii kwa jina Nt'lumant'le Kutila anasema haya ndio Maisha aliyozaliwa na kukulia, anafurahia Maisha ya jamii yake.

Harusi ya kabila la Wahadzabe

Katika hatua ya kutunza jamii yake na kuenzi utamaduni wa jamii hiyo, anasema kama wangeweza kupata maeneo makubwa ya porini ambayo hayaingiliwi na shughuli zingine za kibinadamu.

"Sehemu kubwa ya maisha yetu ni uwindaji, na sisi vijana hupewa mafunzo maalumu na wazee wetu jinsi ya kuwa wanaume hodari na wawindaji." Alisema.

 Kuwa na eneo kubwa kunaweza kuwasaidia jamii hiyo kuweza kurithishana mienendo na mgawanyo wa kimajukumu kijinsia, kutoka jamii.

Wahadzabe ama Wahadza ni kabila la Tanzania  ambalo jamii yake inaishi hasa kando kando ya ziwa Eyasi upande wa kaskazini mwa Tanzania karibu na hifadhi ya Serengeti.

Soma pia:Jamii ya Mbilikimo wa DRC kusaidiwa kiuchumi

Hawana undugu wa karibu na kabila lingine lolote na vile vile lugha yao ni ya kipekee kabisa.

Ni kabila la watu wachache sana jumla yao haizidi watu elfu moja, na inaaminika kwamba wale wanaotegemea Maisha ya uwindaji pekeeni kati ya 200 na 300.

Chakula chao ni mizizi, matunda pori na nyama. Ndilo kabila pekee nchini Tanzania ambalo linaishi kwa mfumo wa Maisha ya watu wa kale.

Mwanamke mmoja wa makamo tukoka jamii ya kabila hili anasema hawahi kabisa kufika mjini na wala hatamani.

"Tunaridhika na Maisha yetu, tunayapenda. Binafsi mimi na wenzangu tunaona hakuna mila zozote ambazo zinatukandamiza sisi wanawake wote tupo sawa.”

Umoja wa Mataifa uliitenga siku hii kama  fursa ya kusherekea utamaduni, kujadili hatua na chanamoto zinazowakabili zinazoakabili jamii za watu wa asili.

Pamoja na mambo mengine jamii hizi, zinatambuliwa kwa mchango wao wa kuenzi tamaduni na kulinda mazingira, lakini hata hivyo bado jamii hizi zinaendelea kuwa masikini na kukabiliwa na hatari za kiusalama.

Wahadzabe walalamika kuhusu uvamizi