Wagombea wote wadai ushindi Madagascar
20 Desemba 2018Wagombea wote katika uchaguzi wa duru ya pili nchini Madagascar wamedai ushindi baada ya uchaguzi huo uliofanyika jana, licha ya kuwa ni asilimia ndogo ya matokeo iliyokwisha tolewa.
Maraisa wawili wa zamani walioshiriki katika uchaguzi wa jana Jumatano wa duru ya pili Marc Ravolomanana na mtu ambaye alimuondoa madarakani mwaka 2009 katika mapinduzi, Andry Rajoelina, na taifa hilo wanamatumaini ya matokeo ya amani na kuturejewa machafuko ya kisiasa ya karibu muongo mmoja uliopita.
Tume ya uchaguzi ya Madagascar imesema matokeo kutoka asilimia 5 ya vituo vya uchaguzi yanaonesha Rajoelina , ambaye namba yake ya kugombea katika orodha ya wapiga kura ni 13, akiongoza kwa asilimia 57.