Waganda watoa heshima za mwisho kwa mwanariadha Cheptegei
14 Septemba 2024Raia wa Uganda Jumamosi ya leo wametoa heshima zao za mwisho kwa Mwanariadha Rebecca Cheptegei aliyefariki baada ya kumwagiwa petroli na kuchomwa moto na mpenzi wake wa zamani.
Mwanariadha huyo wa mbio za marathon mwenye umri wa miaka 33, alikuwa ameshiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Paris ya hivi majuzi.
Soma zaidi.Mwanariadha wa olimpiki wa Uganda afariki baada ya shambulizi la moto
Shambulio hilo la kikatili lilishtua ukanda mzima mashariki mwa Afrika na kuibua hisia kali duniani kote, huku wanaharakati wakilaani kitendo hicho cha unyanyasaji wa kijinsia kilichotokea nchini Kenya.
Mapema leo, wakaazi, maafisa na jamaa walipanga foleni ili kutoa heshima zao katika kijiji cha Bukwo, karibu kilomita 380 kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Uganda, Kampala.