SiasaKorea Kusini
Wafuasi wa Yoon wavamia Mahakama ya Korea Kusini
19 Januari 2025Matangazo
Vurugu hizo zimejiri muda mfupi baada ya mahakama kutangaza uamuzi wa kuendelea kuzuiliwa rumande kwa rais Yoon.
Video zimeonyesha waandamanaji wakitumia vifaa vya kuzima moto dhidi ya polisi waliokuwa wakilinda mlango wa mbele wa Mahakama hiyo, kabla ya kufuliza ndani, kuharibu vifaa vya ofisi.
Soma pia: Mahakama ya Korea Kusini yakataa Rais Yoon kuachiwa huru
Kaimu rais Choi Sang-mok, katika taarifa yake amesema serikali imesikitishwa na matukio ya ukiukaji sheria na vurugu akisema matukio hayo hayakutarajiwa katika taifa hilo la kidemokrasia.
Polisi walirejesha utulivu saa chache baadaye, na kuwakamata waandamanaji 46 na kuahidi kuwasaka wengine waliohusika.