SiasaVenezuela
Wafuasi wa upinzani na serikali kuandamana Venezuela
17 Agosti 2024Matangazo
Kiongozi wa upinzani Maria Corina Machado aliyewataka wafuasi wake kuendeleza mapambano, ameitisha maandamano katika zaidi ya miji 300 nchini Venezuela na hata nje ya nchi, katika kile alichokiita "maandamano ya kutetea ukweli."
Soma pia:Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela awahamasisha upinzani kuendelea kupambana
Venezuela inakabiliwa na mzozo wa kisiasa uliosababishwa na ushindi wenye utata wa rais Nicolas Maduro, katika matokeo ya uchaguzi yaliyokakataliwa vikali ndani na nje ya nchi hiyo.
Idadi ya waliofariki tangu kuanza kwa maandamano
Kufikia sasa, maandamano ya kupinga ushindi wa Maduro yamesababisha vifo vya watu 25 huku wengine karibu 200 wakijeruhiwa na zaidi ya watu 2,400 wakikamatwa tangu ulipofanyikauchaguzi wa Julai 28.