SiasaUfaransa
Wafaransa wajitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi wa Bunge
30 Juni 2024Matangazo
Uchaguzi huo unaweza kushuhudia chama cha mrengo mkali wa kulia cha Marine Le Pen cha National Rally kikichukua madaraka.
Hii itakuwa hatua ya kihistoria kwa chama cha mrengo mkali wa kulia kushinda wingi wa viti bungeni na itakuwa kwa mara ya kwanza nchini Ufaransa tangu uvamizi wa Wanazi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Vituo vya kupigia kura vimefungulia tangu saa mbili asubuhi na vitafungwa saa kumi na mbili jioni.
Rais Emmanuel Macron aliitisha uchaguzi wa mapema baada ya chama chake kupata pigo katika uchaguzi wa Bunge la Ulaya. Wananchi wa Ufaransa wanalalamikia mfumuko wa bei za bidhaa kama chakula na nishati.