Wafanyakazi wa ndani Lebanon wako mashakani - UM
4 Oktoba 2024Matangazo
Taarifa iliyotolewa na Shirika la Uhamiaji la Umoja huo (IOM) imesema baadhi ya wafanyakazi wa ndani wamefungiwa majumbani wakati waajiri wao wakikimbia mashambulizi ya anga ya Israel.
Wengine wametelekezwa mitaani bila ya kuwa na maeneo ya kujihifadhi.
Soma zaidi: Iran yaahidi kuishambulia tena Israel endapo itashambuliwa
IOM imefichuwa madhila wanayopitia zaidi ya wafanyakazi wa kigeni 170,000 waliopo nchini Lebanon, wengi wao wakiwa wanawake kutoka mataifa kama Ethiopia, Kenya, Sudan, Sri Lanka, Bangladesh na Ufilipino.
Shirika hilo limesema hivi sasa linapokea maombi mengi kutoka kwa wahamiaji hao ya kutaka kusaidiwa kurejea makwao.