1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Simu za mkononi za Trump, Vance zadaiwa kudukuliwa

26 Oktoba 2024

Simu za mkononi za mgombea wa urais nchini Marekani kupitia chama cha Republican Donald Trump na mgombea mwenza JD Vance huenda zililengwa na wadukuzi kutoka China.

https://p.dw.com/p/4mFkH
Donald Trump | Mgombea wa urais
Mgombea wa urais nchini Marekani Donald Trump ambaye taarifa zinasema huenda simu yake ilidukuliwa na wadukuzi kutoka ChinaPicha: Alex Brandon/AP Photo/picture alliance

Duru zenye uelewa na suala hilo zimesema wengine waliodukuliwa ni watu wenye uhusiano na mpinzani wa Trump, Kamala Harris, anayegombea urais kupitia chama cha Democratic.

Haikuwekwa wazi mara moja ikiwa kuna taarifa zozote zilizodukuliwa, na maafisa wa Marekani wanaendelea kuchunguza, zimesema duru nyingine zilipozungumza na shirika la habari la AP, ambazo pia hazikutaka kutambulishwa.  

Shirika la Upelelezi nchini Marekani, FBI hata hivyo halikuthibitisha ikiwa Trump na Vance ndio walikuwa walengwa wakuu, ingawa limesema tu kwamba linachunguza.