Wadau wajadili uhuru wa vyombo vya habari Tanzania
3 Mei 2023Katika mbalimbali wamejikita katika kuangalia muskabali wa uhuru wa vyombo vya habari, katika taifa hilo la afrika mashariki ambalo lilishuhudia sheria zilizotungwa zikitumiwa kuminya uhuru wa habari, katika namna iliyotafsiriwa kuwa na nia ya kulinda maslahi mapana ya watawala.
Soma pia: Dunia yaadhimisha Siku ya Uhuru wa Habari
Professor Chris Peter Maina anazitamaza sheria namna zinavyokinzana kati ya Tanzania bara na Zanzibar akisema sheria zinazotungwa katika bunge la Jamuhuri ya muungano wa tanzania zinalenga kutumika pande mbili za nchi lakini zile zinazotungwa na baraza la wawakilishi zanzibar hazitumiki kwa tanzania bara hivyo ametaka kuwa na sauti moja ya sheria itakayotambulika na kutumika kwa pande zote
Waandishi wa habari waliopo kazini wanataja ukinzani kati ya sheria hizo kuwa miongoni mwa changamoto kubwa linapokuja swala la kutekeleza majukumu yao ya kila siku wakitolea mfano baadhi ya mambo yanayokubalika upande wa bara lakini yasiokubalika kwa zanzibar hatua ambayo inawanyima uhuru katika kutekeleza majukumu yao na kutoa wito wakuwepo kwa sheria moja itakayo rahisisha kazi zao za kila siku.
Soma pia: Maoni: Hali ngumu kwa vyombo vya habari Tanzania
Kando na hilo katika mjanda huo wa kitaifa ambao unaendelea baadae leo hii hoja ya kutengwa kwa watu wenye ulemavu linapokuja swala la haki habari linatawala kwa hadhira hiyo hasa viziwi na wasioona vyombo vya habari kama magezi kutozingatia nukta nundu huku program za televisheni zikishindwa kuzingatia viziwi isipokua taarifa za habari pekee.
Msemaji wa serikali ya Tanzania Gerson Msigwa anasema sheria zipo zinazowabana wamiliki wa vyombo vya habari katika kulinda haki habari kwa makundi yote hivyo serikali inazingatia hilo na kuvitaka vyombo vya habari kuzingatia pia.
Kauli mbiu ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari inasema uhuru wa kujieleza kama kichocheo cha haki nyingine za binadamu. Kongamano hili la vyombo vya habari limeandaliwa na wadau wa sekta ya habari, kikiwemo chuo cha mafunzo ya habari cha shirika la Utangazaji la Deutsche Welle, DW Akademie.