Wachunguzi Korea Kusini waapa kumkamata Yoon
1 Januari 2025Wafuasi na wapinzani wa Yoon, aliyeachishwa kazi kupitia kura ya bunge kuhusu jaribio lake la kuondoa utawala wa kiraia mwezi uliopita, wamekita kambi nje ya makazi yake. Amejifungia nyumbani kwake kwa wiki kadhaa akikwepa juhudi za wachunguzi za kutaka kumhoji.
Mkuu wa Ofisi ya Uchunguzi wa Rushwa Dong-woon amewaambia waandishi habari kuwa wanalengakutekeleza agizo la kumkamata rais hiyo bila usumbufu, lakini pia wanashirikiana na polisi na maafisa wengine katika maandalizi. Aidha ameonya kuwa yeyote anayejaribu kuwazuia maafisa kumkamata Yoon atashitakiwa.
Amesema wanavichukulia vitendo kama vile kuweka vizuizi ili kupinga utekelezaji wa waranti wa kumkamata rais huyo kuwa ni kizingiti cha uendeshwaji majukumu rasmi. Haijafahamika kama watafaulu kuitekeleza waranti hiyo ya kumkamata kwa sababu Idara ya Ulinzi wa Rais hapo awali ilikataa kuheshimu hati za kufanywa upekuzi nyumbani kwake.