SiasaChad
Wachad wapiga kura kuhitimisha utawala wa kijeshi
6 Mei 2024Matangazo
Wapiga kura nchini Chad wataamua Jumatatu ikiwa watanue miongo kadhaa ya utawala wa familia ya Deby katika mojawapo ya taifa maskini zaidi duniani ambalo pia limekuwa na umuhimu katika mapambano dhidi ya wapiganaji wenye misimamo mikali katika eneo la Sahel.
Deby anachuana na Success Masra ambaye alikuwa waziri wake mkuu, lakini anatazamwa na wakosoaji kuwa ni kibaraka bila ya kuwepo na wapinzani wengine wakubwa.
Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameonya kuwa uchaguzi huo hautakuwa huru au wa haki kwani mpinzani mkuu wa Deby ameuawa na wengine kupigwa marufuku kugombea.