SiasaAsia
Wabunge wa Marekani wakutana na Dalai Lama
19 Juni 2024Matangazo
Wabunge wanaoongozwa na mbunge Michael McCaul na Pelosi walimtembelea kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 88 nyumbani kwake katika mji wa milimani wa Dharamsala ulioko kaskazini mwa India.
Ziara hiyo inafuatia hatua ya bunge la Marekani kupitisha muswada unaoitaka China ifanye mazungumzo na viongozi wa Tibet.
Soma zaidi: Spika wa bunge la Marekani akutana na Dalai Lama
Ubalozi wa China nchini India umeilaani ziara hiyo ukisema Dalai Lama si kiongozi wa kidini, bali ni mwanasiasa aliye uhamishoni anayehusika na vitendo vya kuipinga China huku akijificha kwenye dini.
Raia wengi wa Tibet walio uhamishoni wanahofia kwamba Beijing itamteuwa mrithi wa Dalai Lama na kuongeza udhibiti wake Tibet.