1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Waasi wa Kihouthi Yemen waziteka afisi za Umoja wa Mataifa

13 Agosti 2024

Waasi wa Kihouthi nchini Yemen wameyavamia makao makuu ya afisi za Shirika la Umoja wa Mataifa katika Mji Mkuu Sanaa na kuchukua stakabadhi, samani na magari.

https://p.dw.com/p/4jQU8
Waasi wa Houthi wa Yemen
Waasi wa Houthi wa YemenPicha: Khaled Abdullah/REUTERS

Waasi wa Kihouthi nchini Yemen wameyavamia makao makuu ya afisi za Shirika la Umoja wa Mataifa  katika Mji Mkuu Sanaa na kuchukua stakabadhi, samani na magari. Haya yamesemwa na afisa mmoja mwandamizi wa Umoja wa Mataifa.

Katika taarifa mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amewataka waasi hao aliowataja kwa jina lao rasmi la Ansar Allah, ambao waliziteka ofisi hizo tangu Agosti 3, waondoke na kurejesha kila walichokichukua mara moja. Hii ni hatua ya hivi karibuni ya waasi hao katika harakati zao za kuwahangaisha watu wanaofanya kazi na mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa nchini humo pamoja na balozi za kigeni.