Mafanikio ya serikali yametoa matumaini ya kumuondoa Assad
29 Desemba 2017Vikosi vya serikali na waasi wa kishia wamewalazimisha waasi wengi kusalimu amri tangu Urusi ilipoingilia kati kwa mashambulizi ya ndege mwaka 2015, na kuwarudisha nyuma waasi katika maeneo madogo madogo. Eneo la Kaskazini Magharibi lililoko karibi na mji wa Idlib, ni moja ya eneo muhimu kwa waasi.
Pia wanadhibiti eneo kubwa linalopakana na Jordan na eneo linalodhibitiwa na Israel la milima ya Golan karibu na Deraa Kusini Magharibi pamoja na maeneo mengine ya Mashariki mwa Ghouta karibu na Damascus. Wapiganaji na familia zao wameanza kuondoka eneo la Beit Jin hii leo ambalo ni kilomita tarkriban 40 kusini Magharibi mwa Damascus, baada ya kupoteza miji hiyo kwa jeshi la Syria na washirika wake kufuatia mapigano makali mapema mwezi huu.
Wapiganaji wengine wameelekea mjini Idlib eneo linalodhibitiwa na wapiganaji wa jihadi na mahali wanakopelekwa watu waioondolewa zamani kwenye maeneo yaliyosalimu amri, na wengine katika maeneo mengine ya waasi kusini-magharibi, yanayodhibitiwa na waasi wa mirengo ya kizalendo.
Beit Jin limekuwa eneo muhimu la kimkakati kutokana na ushiriki wa wanamgambo wa Hezbollah ambao ni maadui wakubwa wa Israel, wanaopigana na waasi katika eneo hilo.
Kusonga mbele kwa jeshi la Syria dhidi ya wanamgambo Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo kulijumuisha mapigano makali ya ardhini na angani yaliyofanyika siku ya alhamisi na Ijumaa hii ikiwa ni kulingana na kundi la uangalizi wa haki za binaadamu la Syria lililo na makao yake nchini Uingereza.
Mkurugenzi wa kundi hilo Rami Abdulrahman amesema mapigano hayo yalisababisha mauaji ya watu 19 leo hasaa katika kijiji cha Abu Dali mjini Idlib baada ya wiki nzima ya mafanikio ya serikali katika maeneo yaliyo karibu na mkoa wa Hama.
Jeshi limefanikia tu kwa mara ya kwanza kuingia mkoani Idlib hivi karibuni, tangu mkururu wa ushindi wa waasi katika eneo hilo kuiondoa serikali mapema mwaka wa 2015. Lakini mafanikio ya serikali katika maeneo mengi yamefifisha matumaini ya waasi kumuondoa Assad kwa nguvu ya kijeshi.
Hii leo ifisi yake imetoa picha ya Assad akikutana na familia moja mjini Homs, katika ishara inayoonyesha kujiamni wakati akiizunguka Syria mwaka huu baada ya miaka kadhaa ambapo alikuwa akibaki mjini Damascus pekee.
Mwandishi: Amina Abubakar/Reuters/AFP/dpa/AP
Mhariri: Iddi Ssessanga