1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Waandamanaji wanaopinga ubaguzi wajitokeza barabarani London

11 Agosti 2024

Waandamanaji wanaopinga ubaguzi wa rangi wamejitokeza barabarani Uingereza kupinga machafuko ya hivi karibuni yaliyochochewa na wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia kufuatia mauaji ya watoto watatu eneo la Southport.

https://p.dw.com/p/4jLcr
England Proteste gegen Rassismus in London
Wanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi nchini Uingereza wamemiminika katikati mwa London kupinga makundi ya siasa kali za mrengo wa kulia. Picha: Tayfun Salci/ZUMA Press Wire/IMAGO

Umati wa watu ulikusanyika mjini London Uingereza, Glasgow Scotland, Belfast Ireland Kaskazini, Manchester na miji mingine ya Uingereza huku kukiwa na hofu ya kutokea makabiliano kati ya waandamanaji hao na makundi yanayopinga uhamiaji.

Soma pia: Mshikamano wa jamii wazima njama za wafanya fujo Uingereza 

Maandamano kama hayo ya kupinga ubaguzi wa rangi na uislamu pia yalifanyika siku ya Jumatano katika maeneo mbalimbali ya Uingereza.

Licha ya hali ya utulivu kuonekana kurudi katika siku za hizi karibuni, vyombo vya habari vya Uingereza vimeripoti kuwa Waziri Mkuu Keir Starmer ameghairi mipango yake ya kuchukua likizo wiki ijayo ili kushughulikia kadhia hiyo.