Vyama vikuu Ujerumani vyazindua kampeni kuelekea uchaguzi
12 Januari 2025Vyama vikuu vitatu nchini Ujerumani vimezindua kampeni kuelekea uchaguzi wa kitaifa utakaofanyika mnamo Februari 23. Wajumbe wa chama cha Social Democratic SPD walikusanyika mjini Berlin, na kumthibitisha Kansela Olaf Scholz kama mgombea mkuu na kupitisha ilani yake ya uchaguzi.
Soma: Uchaguzi Mkuu wa Ujerumani 2025
Nacho chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, cha mbadala kwa Ujerumani AfD pia, kilikutana Jumamosi katika mji wa mashariki mwa Ujerumani wa Riesa kwa mkutano wa siku mbili, ambao ulimchagua kiongozi wa chama Alice Weidel kama mgombea wa ukansela katika uchaguzi ujao.
Takriban waandamanaji 10,000 wanaoipinga AfD walichelewesha kuanza mkutano huo baada ya kufunga barabara.
Nayo kamati tendaji ya chama cha kihafidhina ya CDU, ilikutana kuhitimisha mkutano wake wa siku mbili katika jiji la kaskazini mwa Ujerumani la Hamburg.