1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Von der Leyen kuizuru Poland kutathmini athari za mafuriko

18 Septemba 2024

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, anatarajiwa kuzuru maeneo yaliokumbwa na mafuriko nchini Poland hapo kesho Alhamisi, kwa mualiko wa Waziri Mkuu wa taifa hilo Donald Tusk.

https://p.dw.com/p/4koDs
Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen.
Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen.Picha: FREDERICK FLORIN/AFP

Poland ni moja ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya  katika maeneo ya Mashariki na Ulaya ya Kati yaliyokumbwa na mafuriko tangu juma lililopita.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Czech Petr Fiala, mwenzake wa Slovakia Robert Fico na kansela wa Austria Karl Nehammer wanatarajiwa kukutana katika mkutano wa pamoja na Ursula von der Leyen.

Hayo yanajiri wakati Mji wa mashariki mwa Ujerumani wa Dresden ukiwa katika hatari pia ya kukabiliwa na mafuriko. Kiwango cha maji katika Mto Elbe unaopitia mji huo kimeongezeka na kufikia mita 6 hali iliyoilazimisha serikali kutangaza onyo la pili kubwa la kutokea kwa mafuriko hayo.

Hii inamaanisha maeneo ya makaazi, barabara kuu, na barabara za reli zipo katika hatari hiyo ya kuzidiwa kwa maji.