1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Von der Leyen kufanya ziara mjini Kiev siku ya Ijumaa

19 Septemba 2024

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema atafanya ziara mjini Kiev hapo kesho ili kujadiliana na rais wa Ukraine kuhusu namna ya kuisaidia nchi hiyo katika suala la ugavi wa nishati.

https://p.dw.com/p/4krI0
Ufaransa | PK Ursula von der Leyen katika uwasilishaji wa Tume mpya ya EU huko Strasbourg
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen Septemba 17, 2024Picha: Philipp von Ditfurth/dpa/picture alliance

Von der Leyen amesema Umoja wa Ulaya utatoa nyongeza ya dola milioni 178 kwa Ukraine ili kuisaidia kukarabati miundombinu yake ya nishati iliyoharibiwa na vita, kuanzisha vyanzo vya nishati mbadala pamoja na ujenzi wa makazi. Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA) limesema hivi leo kuwa miundombinu ya nishati ya Ukraine inakabiliwa na shinikizo kubwa kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi ya Urusi kwenye mitambo ya uzalishaji na usambazaji umeme.Hayo yakiarifiwa, Ujerumani imetangaza kuwa mwaka huu itaipatia Kiev msaada wa ziada wa kijeshi wa dola milioni 445 licha ya mzozo kuhusu vikwazo vya bajeti.