1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Von der Leyen asema sauti ya Afrika sharti isikike COP28

5 Septemba 2023

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema sauti ya Afrika ni lazima isikilizwe wakati wa mkutano ujao wa mabadiliko ya tabianchi wa COP28 utakaofanyika huko Umoja wa Falme za Kiarabu.

https://p.dw.com/p/4VzHu
Großbritannien I Ukraine Recovery Conference in London
Picha: Henry Nicholls/AP/picture alliance

Akihutubia mkutano wa Afrika kuhusu mabadiliko ya tabianchi unaoendelea mjini Nairobi nchini Kenya, bibi von der Leyen ameahidi uungaji mkono wa kanda ya Ulaya kwa vipaumbele vya Afrika kuelekea mkutano wa kimataifa wa CO28. 

Von der Leyen amesema mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi unaweza kuwa injini kuu ya ukuaji uchumi wa Afrika na kufikia hilo uwekezaji mkubwa unahitajika. Na Ulaya inataka kuwa mshirika wenu, inataka kuwa mshirika wa kuziba ombwe hilo la uwekezaji.

Guterres aurai ulimwengu kuisaidia Afrika kuwa mzalishaji mkubwa wa nishati jadidifu


Mkutano huo wa Nairobi pamoja na mambo mengine unajadili njia za kuipiga jeki Afrika kufikia uwezo wa kuzalisha nishati ya kutosha kwa kutumia vyanzo visivyoharibu mazingira na kutafuta msimamo wa bara zima kuelekea mkutano wa kilele wa COP28.