Vipi kuziba bomba la mafuta linalovuja Ghuba la Mexico ?
28 Mei 2010Bado haijulikani iwapo hatua za kampuni la mafuta la BP ilizochukua kuzuwia kuvuja kwa mafuta kutoka bomba lake la chini ya bahari huko Ghuba la Mexico, limefaulu. Kwa kumwaika mamilioni ya lita za mafuta baharini ,Rais Barack Obama, anaezuru leo eneo hilo kujionea kwa macho yake uchafuzi wa mazingira ,anajikuta katika shinikizo kubwa. "Msiba huu wa kuvuja mafuta ni "msiba wa Katrina kwa Rais Obama".Hivyo ndivyo inavyosemekana hivi sasa ikilinganishwa na uzembe ilioufanya utawala wa George Bush, 2005 katika kukabiliana haraka na kimbunga cha Katrina:
Hakuna anaeweza kumtupia Barack Obama, jukumu la kuwa ni chanzo cha balaa hilo la kuvuja mafuta katika Ghuba la Mexico,nje ya pwani ya Marekani.Kwani, ni matokeo ya uzembe na ujeuri wa mtangulizi wake Ikulu.Lakini, akiwa rais ,anabidi sasa kukabili jukumu lake.Chanzo cha msiba huu kinalingana na ule msiba wa kimbunga wa "Katrina" pale kinga za mwambao wa pwani zilizokuwa zihimili dharuba ziliposhindwa kuzuwia mafuriko.
Na sawa kama wakati ule wa Rais George Bush, sasa rais Barack Obama , hakufaulu kuwaridhisha wananchi kwamba ameidhibiti hali ya mambo.Alichukua siku 38 kabla kuitisha mkutano na waandishi habari kuzungumzia msiba uliozuka katika Ghuba la Mexico.
Picha zinazoonesha watu hadharani ,mashini au marekebu zikipambana na uchafuzi wa mazingira kutokana na kuvuja kwa mafuta hazipo. Picha za kinga zinazoelea majini kuzuwia uchafuzi wa kingo za bahari ,zinaoonekana zikiwa na lengo la kuwatia watu kitunga cha macho kuwa, hatua zinachukuliwa kurekebisha mambo.Hatua hizi ni jibu la filamu za waandishi habari waliovaa glovu mikononi wakishika matope ya mafuta yanayoelea majini au picha za wavuvi waliofadhahika hawajui vipi wataweza kuishi.
Juu ya hayo yote, zinaibuka pia taarifa za kutatanisha: Kwa upande mmoja , Kampuni la petroli la BP kwa muujibu alivyoeleza Rais Obama, si ruhusa kuchukua hatua za kupambana na uchafuzi uliozuka bila idhinmi ya serikali ya Marekani.
Kwa upande mwengine, Rais Obama anaungama kuwa utawala wake hauna maarifa ya kukabiliana na kuvuja kwa mafuta ya petroli kazika kina cha chini kabisa cha bahario.Na ndipo hapo palipo na tofauti kati ya ule msiba wa kimbunga cha Katrina na huu wa mafuta:
Kwani, hata ingelikuwa Rais Obama alitaka, serikali yake isingemudu kuchukua hatua za kuliziba bomba linalovuja mafuta chini kabisa ya kina cha bahari.Sio tu haikuwa na haki kisheria kuchukua jukumu hilo, bali isingeweza pia hata kutumia jeshi lake la wanamaji.Wanajeshi wa Marekani, wapigana vita jangwani,milimani na angani,lakini vita vya kupambana na bomba la mafuta linalovunja mita 1.500 chini kabisa ya bahari,hawaviwezi.
Kinyume na msiba wa kimbunga cha Katrina.Kwa hali ile ya dharura iliozuka kupitia msiba wa kimaumbile ,ni ruhusa kulitumia Jeshi la taifa .Madhambi ya 2005 yalitokana na uzembe wa kuongoza juhudi za uokozi,kutopima hali ipasavyo na uongozi dhaifu wa utawala wa George Bush.
Mkasa wa BP wa kuvuja mafuta ,kinyume chake, unadhihirisha ukosefu wa sheria maalumu za kuyadhibiti mashirika ya mafuta pamoja na shughuli zao na ubepari unakoongoza.Kiroja cha mambo, ni wanasiasa wale wale wanaomtuhumu Obama kuwa ni msoshalisti, ndio wale wale, wanaodai serikali yake iiingilie kati.
Mwandishi: Bergmann,Christina (DW Washington)
Mtayarishi: Ramadhan Ali
Imepitishwa na Hamidou Oummilkheir