Viongozi watoa wito kuvaa kibandiko cha Kippa cha Wayahudi
31 Mei 2019Baraza la Wayahudi nchini Ujerumani linakosoa kwamba hayo ni maandamano ya propaganda ya Waislamu dhidi ya Israel kwa kile wanachokiita kutaka kuupora mji wa Jerusalem na kuifuta Israel kutoka katika ramani ya dunia. Al Quds ni jina la Kiarabu kwa mji wa Jerusalem. Wakati wa maandamano hayo kutakuwa na maandamano ya kupinga.
Afisa anayehusika na kupambana na chuki dhidi ya Wayahudi katika serikali ya Ujerumani Felix Klein , ametoa wito kabla ya maandamano kila mtu avae kofi ya Kiyahudi kama ishara ya mshikamano na Wayahudi na kupinga maandamano ya Al-Quds. Siku chache zilizopita hata hivyo alisababisha kuwamo katika vichwa vya habari vya vyombo mbali mbali, pale alipowaonya Wayahudi dhidi ya kivaa kibandiko hicho hadharani kila mahali nchini Ujerumani.
Ukweli ni kwamba idadi ya matukio ya chuki dhidi ya Wayahudi inapanda. Takwimu za kihalifu zinaeleza kwamba mwaka uliopita matukio 1799 yalifanyika kuhusiana na chuki dhidi ya Wayahudi.
Hii ni karibu asilimia 20 zaidi ya mwaka 2017. Klein alitoa matamshi yake kwa msingi wa matukio haya ya kihalifu yakiongezeka katika jamii bila ya kudhibitiwa pamoja na matukio ya kikatili, na kuwa chachu ya chuki dhidi ya Wayahudi.
Onyo kwa Wayahudi
Klein amefafanua kwamba mtandao wa internet na mitandao ya kijamii imechangia kwa kiasi kikubwa, lakini pia mwendelezo wa mashambulizi ya kumbukumbu ya utamaduni wetu.
Rais wa Israel amekasirishwa na onyo alilotoa Klein na kukosoa kile alichosema , kusalimu amri kwa wenye chuki dhidi ya Wayahudi nchini Ujerumani.
Kwa mara nyingine tena wayahudi hawana uhakika wa usalama nchini Ujerumani.
Afisa anayehusika na mapambano ya kupinga chuki dhidi ya wayahudi katika jamii ya Wayahudi mjini Berlin Sigmount Koenigsberg, hayachukulii matamshi ya Klein kama kusalimu amri , badala yake ni kama wito wa kuwa macho, ambao pamoja na hayo ni dhaifu na kwamba umetolewa kwa njia mabyo haistahili. Ningetarajia , kwamba aongeze kuwa kila kitu kitafanyika ili kila Myahudi nchini Ujerumani na kila siku na hata nyakati za usiku anaweza kuvaa kibandiko hicho Kippa.
Kwa hiyo kungekuwa na tamko la kupambana dhidi ya watu wenye chuki dhidi ya wayahudi, amesema Koenigsberg.
Muda wa kuchukua hatua
Jamii ya Wayahudi nchini Ujerumani inaitaka serikali ya Ujerumani kufanya mazungumzo nayo. Muda umepita wa kuchukua hatua , kwa kuwa wayahudi katika baadhi ya maeneo ya miji mikubwa wako katika hatari, kwabababu wanatambulika kama Wayahudi, anasema rais wa baraza kuu la wayahudi, Josef Schuster. Amekwisha kuwa katika hali hiyo miaka miwili iliyopita.
Anakaribisha, hatua kama hizo, iwapo ngazi ya juu ya viongozi wa kisiasa wataliangalia kwa makini, anasema Svhuster.
Mapambano dhidi ya chuki kwa wayahudi ni lazima yawe mapambano ya jamii yote, anasisitiza. Hali ya matumizi ya nguvu ya kisiasa inaonekana kushika kasi.
Hata hivyo maandamano ya mjini Berlin ya kile kinachoitwa al-Quds si maandamano ya chuki dhidi ya wayahudi, haya ni maandamano yaliyopangwa kudai haki kwa Wapalestina. Pamoja na kudai haki kwa Wapalestina lakini bila kuangalia upande wa pili yanaweza kuwa pia chuki dhidi ya Wayahudi.
katika mjadala kuhusu kuvaa kibandiko cha kitamaduni cha wayahudi Kippa , rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ametoa wito watu wote watakaoshiriki katika maandamano hayo mbadala wavae kibandiko hicho , ili kupambana na chuki dhidi ya wayahudi.