1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa ulimwengu waanza kuwasili London kumuaga Malkia

17 Septemba 2022

Viongozi wa ulimwengu wameanza kukusanyika mjini London kuanzia leo Jumamosi kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II.Wana mfalme William na Harry watatoa heshima zao kwa bibi yao.

https://p.dw.com/p/4H0Fs
Großbritanien I Royale Totenwache I Queen
Picha: Yui Mok/AP/picture alliance

Leo Jumamosi wana mfalme William na Harry wakitarajiwa kuwaongoza wajukuu zake Malkia kwenye shughuli ya kutoa heshima zao za mwisho kwenye jeneza lake. Siku ya Ijumaa Mfalme wa Uingereza Charles wa tatu na ndugu zake walisimama karibu na jeneza la mama yao marehemu Malkia Elizabeth wa pili kutoa heshima zao huku maelfu ya waombolezaji wakiwa kwenye foleni ndefu wakisubiri nao kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi wao.

Mbele Mwanamfalme Wlilliam na nyuma yake ni Mwanamfalme Harry
Mbele Mwanamfalme Wlilliam na nyuma yake ni Mwanamfalme HarryPicha: Alkis Konstantinidis/AP/picture alliance

Walielezwa kwamba huenda wangelisubiri kwenye foleni hiyo kwa saa 24 kabla ya kupata fursa ya kumuaga Malkia Elizabeth wa pili. Mistari hiyo ni mirefu mno kando ya Mto Thames tangu siku ya Jumatano wakati jeneza la malkia Elizabeth wa pili lilipoletwa kwenye jumba la bunge la Uingereza, Westminster. 

Mfalme Charles wa tatu, Princess Anne, Prince Andrew na prince Edward, wakiwa wamevalia sare za kijeshi, walisimama kimya na kuinamisha vichwa vyao kwa dakika 15 katika Ukumbi wa kihistoria wa Westminster ambapo jeneza la marehemu malkia wa Uingereza limewekwa hapo tangu siku ya Jumatano kwa ajili ya kuagwa kabla ya kuzikwa hapo siku ya Jumatatu tarehe 19.

Kifo cha malkia huyo wa Uingereza kilitokea mnamo Septemba 8 akiwa na umri wa miaka 96, baada ya kutawala kwa miaka 70 kwenye kiti cha enzi.

Mfalme Charles lll na ndugu zake Prince Andrew na Prince Edward wakiwa kwenye kasri ya Wstminster mjini London ambako mwili wa Malkia umelaazwa kwa ajili ya watu kutoa heshima zao kabla ya mazishi.
Mfalme Charles lll na ndugu zake Prince Andrew na Prince Edward wakiwa kwenye kasri ya Wstminster mjini London ambako mwili wa Malkia umelaazwa kwa ajili ya watu kutoa heshima zao kabla ya mazishi.Picha: DANIEL LEAL/POOL/AFP

Mrithi wa malkia, Mfalme Charles III, atakutana Jumamosi na mawaziri wakuu wa mataifa ya Jumuiya ya Madola ambayo ni makoloni 14 ya zamani ya Uingereza. Australia, New Zealand na Kanada, zimemtangaza rasmi kuwa Mfalme Charles wa tatu kuwa ni mtawala wao mpya.

Umma una hadi Jumatatu asubuhi kulitazama jeneza la Malkia Elizabeth wa pili kabla ya kufanyika mazishi ya kwanza ya kiserikali nchini Uingereza kwa karibu miongo sita.

Mfalme wa Uingereza Charles lll
Mfalme wa Uingereza Charles lllPicha: HANNAH MCKAY/POOL/AFP

Hafla hiyo ya kuuga mwili wa Malkia itafanyika katika kanisa la Westminster Abbey na inatarajiwa kutazamwakwenye runinga na mamilioni ya watu duniani kote. Wageni zaidi ya 2,000, wamealikwa isipokuwa viongozi kutoka nchi zinazozozana na Uingereza kama Urusi, Belarus na Afghanistan hawakualikwa. Mazishi ya faragha yatafuata katika kasri ya Windsor baada ya ibada.

Chanzo:AFP