Viongozi wa Ulaya wanajadiili njia za kuzalisha nishati
25 Aprili 2023Viongozi wa nchi tisa za Ulaya wamekutana kujadili njia za kuzalisha nishati inayotokana na nguvu ya upepo kutoka bahari ya kaskazini. Mkutano wa viongozi hao unafanyika wakati ambapo nchi za Ulaya magharibi zinajaribu kuondokana na kuitegemea Urusi kwa mahitaji yao ya nishati. Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na rais wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya pia wamehudhuria mkutano huo uliofanyika kwenye mji wa bandari wa Ostend nchini Ubelgiji. Umoja wa Ulaya unaazimia kufikia lengo la asilimia 42 ya nishati endelevu hadi utakapofika mwaka 2030. Waziri mkuu wa Denmark Mette Frederiksen amesema kikao chao kimetoa ishara thabiti katika kufikia lengo la kuzalisha nishati bila ya hewa chafuzi ya kaboni hadi hapo mwaka wa 2050. Gharama za mradi huo zinatarajiwa kufikia Euro bilioni 800.