Viongozi wa Ulaya kukutana kujadili uhamiaji haramu
10 Desemba 2024Viongozi hao wanatarajia kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano wao katika mapambano dhidi ya makundi ya uhalifu yanayohusishwa na vitendo vya uhamiaji haramu barani Ulaya. Viongozi hao watajadili pia namna ya kuzidisha juhudi zao ili kuyadhoofisha makundi ya magendo na kuhakikisha wote wanaohusika na shughuli hizo hatari wanafikishwa mahakamani.
Soma pia: Umoja wa Ulaya wajizatiti zaidi juu ya wahamiaji haramu
Wawakilishi wa Tume ya Ulaya na shirika la kulinda mipaka ya Ulaya Frontex na lile la Polisi ya Ulaya Europol watashiriki pia mkutano huo ili kuelezea mpango kabambe wa utekelezaji wa hatua hizo kwa mwaka ujao wa 2025. Tangu kuanza kwa mwaka huu, takriban wahamiaji 34,000 wamewasili Uingereza wakipitia baharini kwa kutumia mashua na karibu watu 70 wameripotiwa kufa maji.