Viongozi wa Magharibi wakusanyika kukumbuka D-Day
6 Juni 2024Maadhimisho hayo yanafanyika wakati ambapo vita vipya vimeligubika bara la Ulaya kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Soma pia: Dday ni tukio muhimu la kijeshi lililotuondolea wanazi Ujerumani-Merkel
Mwenyeji wa hafla hiyo, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa anaungana na Rais Joe Biden wa Marekani, Mfalme Charles wa Tatu wa Uingereza, Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, na viongozi wengine kukumbuka ushujaa wa maafisa wa vikosi washirika waliopoteza maisha yao mnamo Juni 6, 1944, ili kuikomboa Ulaya kutoka kwa wavamizi wa Wanazi.
Soma pia:
Maoni: Mafunzo kutoka vita kuu ya II ya dunia
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz pia ni miongoni mwa walioalikwa.
Hata hivyo, hakuna afisa yeyote wa Urusi aliyealikwa, licha ya mchango mkubwa wa jeshi lake kwenye kuushinda utawala wa kinazi wa Ujerumani.