Viongozi wa G7 kujadili "mabavu ya kiuchumi" ya China
13 Mei 2023Matangazo
Hayo yameelezwa na afisa mmoja wa Marekani anayefahamu ajenda za mkutano ujao wa G7 utakaofanyika Mei 19 hadi 21 huko Hiroshima nchini Japan.
Kulingana na afisa huyo viongozi wa G7 wanataka kuzuia kile wanachokiita "mabavu ya kiuchumi" ya China na tabia nyingine yoyote ya Beijing inayotia mashaka.
Nguvu za kiuchumi za China na udhibiti iliyonayo kwenye teknolojia mamboleo vimekuwa masuala yanayotoa kitisho kwa mataifa ya G7 ambayo yana mafungamano makubwa ya kiuchumi na China.
Mbali ya masuala ya kiuchumi, viongozi wa G7 watajadili pia nafasi na dhima ya China katika maeneo mengine ikiwemo mabadiliko ya tabianchi.