1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa EU kujadili hali ya kiuchumi wa kikanda

24 Machi 2023

Viongozi wa Umoja wa Ulaya watakutana tena leo Ijumaa kwa siku ya pili ya mkutano wao wa kilele kujadili hali ya kiuchumi katika ukanda huo baada ya kushuhudiwa msukosuko wa kifedha katika sekta ya kibenki duniani.

https://p.dw.com/p/4PAY8
Belgien EU l Treffens der Außenminister der Europäischen Union in Brüssel
Picha: Johanna Geron/REUTERS

Viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya zinazotumia sarafu ya Euro watakutana pamoja na rais wa benki kuu ya Umoja huo, Christine Lagarde, mjini Brussels kujadili hali ya kifedha katika ukanda huo.

Mazungumzo hayo yanakuja baada ya kupandishwa kwa mara nyingine viwango vya riba na benki hiyo katika juhudi za kupunguza mfumko wa bei na kutokana na wasiwasi juu ya athari zitakazosababishwa na hatua ya hivi karibuni ya kuporomoka kwa benki kubwa ya Credit Suisse ya nchini Uswisi.

Soma pia: Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamualika Guterres katika mkutano wao wa kilele

Hatua ya kupunguzwa kwa kiasi kikubwa usambazaji wa gesi ya Urusi kutokana na Umoja wa Ulaya kuiwekea vikwazo nchi hiyo, kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine, imesababisha bei za nishati kuongezeka na kusababisha khofu ya kutokea mporomoko wa kiuchumi. Mkutano huo pia utajadili vita vya Ukraine.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW